Eneza habari humu duniani. Po pote panapo moyo wa huzuni; Ndimi za Wakristo zitangaze Neno, Yupo Mfariji. Yupo Mfariji, yupo Mfariji, Roho Mtakatifu ndiye Msaidizi; Eneza habari humu duniani. Yupo Mfariji. Mfalme wa wafalme, Yesu, umtazame Ametuletea siha ya milele; Mateka wapate Ukombozi wake Yupo Mfariji. mmon Viwezeje mimi kutamka vizuri Kumsifu Mwokozi aliye mbinguni? Nitangaze sasa, neno la furaha Yupo Mfariji. Wenzangu, tuimbe nyimbo za milele; Mbinguni tujaze na shukrani tele; Upendo wa Bwana ujulike sana, Yupo Mfariji.